Saturday, January 3, 2009

Mwl.A .Chiwalala atunikwa tuzo la Sanaa Finland






Ninayoheshima na furaha kuwataarifu kwamba Arnold Chiwalala mwanamuziki/mwalimu wa Kitanzania anayechukua Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Cha Muziki Cha Sibelius (Sibelius Academy) ametunukiwa Tuzo ya Dhahabu ya muziki wa Ala ya Kantele 2008. Kantele ni ala ya kiasili ya Finland. Tuzo hii hutolewa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni ya Finland kwa mwanamuziki bora ambaye amechangia katika utunzi(composition) na uendelezaji (promotion) wa ala ya Kantele ndani na nje ya Finland.

Arnold Chiwalala ni muhitimu na mwalimu kutokea Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Vile vile ni mwanamuziki, mtunzi, muandishi wa nyimbo na mbunifu wa miondoko (choreographer). Kazi za Mwalimu Chiwalala zinatambulika kimataifa ambapo ameshiriki katika warsha, matamasha na makongamano sehemu mbali mbali ulimwenguni ikiwemo Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Uingereza, Ujerumani, Marekani, Urusi, Norway, Denmark,Sweden,Finland, Estonia na Yugoslavia.
contact.Arnold Chiwalala email, achiwala@siba.fi, Simu +358405290622

Nakutakia kazi njema na kila la heri katika mwaka mpya wa 2009.
( katika picha wa kati ni Mwl Anorld chiwalala na Menard mponda,Ricardo padilla,Aliko Mwakanjuki na Topi korhonen katika kazi mbali zikiwemo Bandubandu,Sisi Njia panda na Chizentele kazi zote hizi zilitumia takribani miaka Mitano na kum wezesha Mwl kuatunikwa tuzo Nishani ya dhahabu mwaka 2008.

No comments: